Jeremiah 3:2-7


2 a“Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone.
Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe?
Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi,
ukakaa kama yeye ahamahamaye jangwani.
Umeinajisi nchi
kwa ukahaba wako na uovu wako.

3 bKwa hiyo mvua imezuiliwa,
nazo mvua za vuli hazikunyesha.
Hata hivyo, una uso usio na haya kama wa kahaba;
unakataa kutahayari kwa aibu.

4 cJe, wewe hujaniita hivi punde tu:
‘Baba yangu, rafiki yangu tangu ujana wangu,

5 dje, utakasirika siku zote?
Je, ghadhabu yako itaendelea milele?’
Hivi ndivyo unavyozungumza,
lakini unafanya maovu yote uwezayo.”

Wito Kwa Ajili Ya Toba

6 eWakati wa utawala wa Mfalme Yosia, Bwana aliniambia, “Umeona kile Israeli asiye mwaminifu amekifanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko. 7 fMimi nilifikiri kuwa baada ya kuyafanya yote haya angelinirudia, lakini hakurudi, naye dada yake Yuda mdanganyifu aliona hili.
Copyright information for SwhKC